Burudani

Sony wasitisha kutoa filamu ya komedi ‘The Interview’ iliyohusu mpango wa kumuua kiongozi wa Korea Kaskazini

Kampuni ya Sony Pictures Entertainment imesitisha kutoa filamu yake ya komedi, The Interview ambayo inazungumzia mkasa wa kutunga unaohusu mpango wa kumuua kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un.

the-interview-2014.31431

Kampuni hiyo ilikuwa ifanye uzinduzi wa filamu hiyo siku ya Christmas lakini hackers walitishia kufanya shambulizi kama la 9/11 kwenye majumba ya sinema ambayo yangeionesha nchini Marekani.

Serikali ya Marekani jana ilithibitisha kuwa Korea Kaskazini imehusika kwenye udukuzi huo ulioshuhudia kuvuja kwa emails za ndani na za siri kutoka Sony katika wiki mbili zilizopita.

Wapelelezi wa Marekani wamebaini kuwa udukuzi huo dhidi ya mifumo ya Sony ni kazi ya watu wanaofanya kazi kwa niaba ya serikali ya Korea Kaskazini. ‘Sony Pictures haina mpango wa kuitoa tena filamu hiyo,” msemaji wake alisema jana. Utengenezaji wa filamu hiyo umegharimu dola milioni 42.

Serikali ya Marekani inatarajia kutoa tamko kuhusiana na suala hilo leo na kuamua kama ichukue uamuzi wa kuishutumu rasmi Korea Kaskazini kwa kufanya shambulio la kigaidi ama la.

Kwenye mahojiano aliyofanyiwa na kituo ABC jana, Rais Barack Obama alisema watu wanaweza kuendelea kwenda kwenye majumba ya sinema lakini akasisitiza kuwa vitisho hiyo ni ‘serious’.

Watu wengi huko Hollywood wamechukizwa na hatua hiyo ya kuisitisha filamu hiyo na wametumua Twitter kuelezea hasira yao.

Bofya hapa kusoma mkasa mzima wa udukuzi (hacking) kwenye computer za Sony.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents