Burudani

Sony Music Africa kumtangaza msanii wake mpya wa Tanzania hivi karibuni, Je ni Ali Kiba?

Label ya Sony Music Africa itamsaini msanii wa pili wa Tanzania atakayeungana na Rose Muhando mwishoni mwa mwaka huu. Mkurugenzi na Mkuu wa Vipaji na Biashara Mpya Afrika wa Rockstar 4000 / Sony Music Africa, Seven Mosha aliiambia Bongo5 kuwa msanii huyo atatangazwa baada ya nyimbo za Rose Muhando aliyesainishwa February mwaka jana zitakapoanza kutoka.

IMG_2606
Seven Mosha akiwa na Vanessa Mdee

Tayari Rose Muhando ameshaachia video ya wimbo wake uitwao Wololo na hiyo inaashiria kuwa tangazo la msanii huyo mpya linaweza kufanywa siki si nyingi na kama si mwezi huu mwishoni basi inaweza kuwa mwanzoni mwa January.

Akielezea vigezo wanavyotumia kuwasainisha wasanii kwenye label hiyo, Seven alisema mara nyingi hawachukui wasanii wasiojulikana kabisa na hutumia zaidi mtandao kujua msanii anayefaa.

“Kila Jumatano huwa tuna meeting inayoitwa A&R ambayo wanaangaliwa wasanii wote waliopo online,” alisema Seven. “Kitu cha kwanza ambacho huwa tunaangalia ni online. Ntachukulia mfano Xtatic. Ilikuwa ni kazi aliyoitoa as underground akaweka video yake online and the alikuwa hajulikani, hana deal yoyote lakini kukawa kuna watu wameupenda wimbo wake, wameappreciate talent yake.”

“Basi tukiona hivyo na tukiangalia overall vitu vingine vinakaa sawa, unakuta labda Xtatic ni mtu ambaye ana muonekano mzuri, anaandika nyimbo zake mwenyewe, anaweza kuimba lugha tofauti, labda anaweza kuplay instruments vilevile. Kwahiyo inakuwa ni mtu ambaye ni rahisi sana kumwekea investment, ni rahisi sana kumuuza. Lakini unakuta kuna wengine ambao wameshaanza kibiashara kwa lengo fulani , ndio watu kama D’Banj, kama Rose Muhando, unaona kwamba hiki ni kipaji kitakakaa kwa muda fulani, kwahiyo sisi tukiongeza ujuzi wetu tutaenda mbali pamoja naye.”

Seven alisisitiza umuhimu wa wasanii kupatikana mtandaoni kwakuwa ni kigezo kikubwa zaidi.

“Muda mwingi sana tunautumia online, different websites, different Youtube links. Saa zingine kwenye Twitter unakuta mtu amemrecommend sana mtu huyu, tunasikiliza nyimbo. Kama tunakupenda tukupigia simu, first meeting inafanyika, tunaangalia kama una malengo kama yetu, basi unasainishwa. Digital platform ni kitu kikubwa sana kwetu. Ndio tunaangalia sana vitu vingi huko.”

1c764f48665311e3b5aa12644b575dea_8

Wakati ambapo wapenzi wengi wa muziki wa Tanzania wana hamu ya kufahamu ni msanii gani huyo atakayetangazwa na Sony Music Africa, kuna dalili nyingi kuwa msanii huyo anaweza kuwa Ali Kiba. Kuna sababu nyingi za Ali Kiba kuwa ndio msanii atakayetangazwa ikiwa pamoja na ukaribu alionao na kampuni ya Rockstar 4000 ambayo ilimchukua miaka miwili iliyopita ikishirikiana na Airtel na Sony Music Africa kwenye project ya One 8 ambapo aliungana na wasanii wengine wa Afrika wakiwemo 4×4, 2Face, Amani, Fally Ipupa, JK, Movaizhaleine na Navio na kurekodi wimbo uitwao ‘Hands Across the World’ waliomshirikisha R.Kelly.

Bila shaka tangu project hiyo, bado Sony Music Africa wameendelea kuwa karibu na Ali Kiba na pengine ukaribu huo ndio uliosababisha ukimya wa hitmaker huyo wa Single Boy miaka ya hivi karibuni.

1526571_629821603742799_839440795_n
Redsan, producer wa Homeboyz Productions, Sappy na Ali Kiba

Dalili nyingine ni ile collabo anayofanya pamoja na Redsan ambaye naye alisainishwa na Sony Music Africa hivi karibuni.

Kwakuwa Ali Kiba ameonesha kupunguza kasi kimuziki nchini, huenda anaweza akarudi tena na moto zaidi baada ya deal yake na Sony Music Africa ikitangazwa rasmi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents