Burudani

Songa: Sina stress muziki usiponipa mkwanja!

Rapper Songa amesema haimuumizi kutoingiza pesa kwenye muziki wake kwakuwa furaha yake ya kweli ni kuona watu wanakubali muziki wake.

One akiwa na Songa

Songa ameiambia Bongo5 kuwa muziki anaofanya ni kwaajili ya mashabiki wa muziki wake.

“Hainipi wakati mgumu na haitakuja kunipa wakati mgumu,” amesema rapper huyo wa Tamaduni Muzik.
“Mimi nafanya muziki kwa sababu napenda na pia napenda kuona watu wanafurahia ninachokifanya. Kwahiyo kwakuwa mwanzo sikuanza kwaajili ya kufanikiwa au kupata hela kihivyo, haijalishi mtu mwingine anakuja kufanya vipi, ilimradi naamini mimi nafanya bora na huyo mwenza anafanya bora japo tunafanya vitu viwili tofauti. Kila mtu anafanya chake hatuwezi kufanya kitu kimoja. Kwahiyo furaha ni kuona nafanya hivyo.”

Katika hatua nyingine Songa amesema yupo njiani kutoa video ya wimbo wake mpya ‘Beef’.

“Wimbo wangu mpya ‘Beef’ umetoka last week na wadau wameupokea vizuri na nafurahi kwa hilo. Lakini natarajia kuachia video next week au baada ya wiki mbili zijazo nitaachia video ya huu wimbo Beef ambao tayari upo bado issue za ku-edit kama hivyo kwahiyo watu wakae tayari kuna mambo mengi yanakuja.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents