Diamond Platnumz

Song: Ney wa Mitego ft Diamond – Muziki gani – Hip Hop vs ‘wabana pua’

Ni brand new track kutoka kwa Ney wa Mitego akiwa amemshirikisha Diamond Platnumz, ‘MUZIKI GANI’. Ukiwa na saa chache tu tangu utambulishwe wimbo huu tayari umeshakuwa gumzo.

Nay na Diamond

Huu ni wimbo wenye idea unique kwakuwa wasanii hawa wawili wameamua kuimba kwa kuwakilisha makundi mawili ya wasanii nchini, wale wanaofanya Hip Hop wanaowakilishwa na Ney na wale wanaofanya muziki wa kuimba wakiwakilishwa na Diamond.

Akiongea kwenye interview ya XXL, Ney amesema huo ni wimbo wenye reality kuliko zote zilizowahi kutoka kwakuwa ameyasema mabaya ya Diamond ikiwa pamoja na mtindo wake kuwa na uhusiano na wasichana kibao. “Mbona unawachezea unawatema kama BIG G, mara Wema, mara Jokate, mara Naj mara Penny, je mnafanya muziki ili mpate mabinti,” yanasema mashairi ya Ney.

Chorus imeimbwa kwa mabishano kati yao inayosema:

Diamond: Hivi nyie mamc mnachoimba vitu gani, mara bange mara matusi sasa ndio muziki gani?
Ney: Hii ni Hip Hop HOP wahasisi wa burudani tushachoka kutoa mapenzi kabana pua nyumbani.

Ney pia anamshambulia Diamond kwa kumwambia, “ Q Chilla analalama anasema umemroga, mganga wako aliyekutoa umemkimbia hujamlipa.”

Ngoma itahit bila wasiwasi.

Download Hapa

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents