Michezo

Soka Ulaya: Real Madrid yanyukwa na Sevilla, Man City hoi kwa Everton

Vinara wa ligi kuu ya Hispania, Real Madrid walionja shubiri ya kupoteza mchezo baada ya kuambulia kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa wanaoshika nafasi ya pili Sevilla.

Mabao ya Sevilla yalipachikwa kimiani na Sergio Ramos aliyejifunga huku bao la ushindi likiwekwa kimiani na mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Man City, S.Jovetic. Awali Real walianza kufunga kupitia kwa Cristiano Ronaldo aliyepachika goli kwa mkwaju wa penalti.

Huo unakuwa mchezo wa kwanza kwa Real Madrid kupoteza, baada ya kucheza michezo 40 katika mashindano yote na kutopoteza. Matokeo hayo yanaicha Real Madrid wakiwa bado vinara wa La Liga kwa kuwa Nna pointi 40, wakifutiwa na Sevilla yenye pointi 39 na Barcelona wakiwa nafasi ya tatu wakiwa na pointi 38, huku Barca na Sevilla zikiwa zimecheza mchezo mmoja zaidi.

Kwingineko nchini England, kocha wa kihispania Pep Gurdiola aliambulia kipigo kikali zaidi kuwahi kukipata katika maisha yake ya soka baada ya kutandikwa mabao 4-0 kutoka kwa klabu ya Everton ya Koeman. Matokeo hayo yanaiacha Manchester City ikiwa nafasi ya tano, nafasi mbaya zaidi timu inayoongozwa na Pep kuwa nayo katika wakati kama huu wa msimu.

Mechi nyingine miamba ya soka la England Liverpool na Manchester United walitoshana nguvu kwa kutoa sare ya 1. Magoli yalifungwa na Milner aliyeanza kufunga kwa mkwaju wa penalti na Zlatan Ibrahimovic kusawazisha kwa kichwa dakika za mwishoni mwa mchezo.

By Eliezer Gibson greencitynative
IG:gibson_elly

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents