Technology

Smart toothbrush: Mswaki unaompa taarifa mtumiaji kupitia smartphone wakati wa kusafisha kinywa

Wale mnaopenda vitu smart, kama smartphone, smartwatch, smarthome, sasa mnaletewa smart toothbrush, mswaki ambao unauwezo wa kutoa taarifa kwa mtumiaji kupitia simu ya mkononi.

Smart toothbrush

The Kolibree toothbrush imetengenezewa kifaa maalum (sensor), na inatumia app kumuonesha mtumiaji kila sehemu mswaki huo unapopita kinywani na kumshtua endapo ataruka sehemu.

Pia mswaki huo unamjulisha mtumiaji kama amesafisha kinywa kwa muda wa kutosha na kama amesafisha sehemu zote muhimu za kinywa.

Smart toothbrush2

Taarifa zote kutoka kwenye mswaki huo zitaonekana katika smartphone ya Android na iOS ya mtumiaji kwa kupitia bluetooth.

Smart toothbrush zitaanza kuuzwa baada ya April mwakaa huu kwa $100.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents