Burudani

Skylight Band: Ni kweli tuliwatikisa Machozi Band (Audio)

Skylight Band wamekiri kuwa wao ni chanzo cha kushuka kwa umaarufu wa Machozi Band.

20219_10151127562712864_1000617387_n

Meneja wa bendi hiyo, Aneth Kushaba ameiambia Bongo5 kuwa kuchukua waimbaji wawili kutoka Machozi Band kulikuwa na madhara makubwa kwa bendi hiyo inayomilikiwa na Lady Jaydee.

“Ni kweli kwasababu wale ni wasanii wanaojiweza ndio walikuwa wasanii nguzo ya Machozi. Kwahiyo walipokuja Skylight, lazima kama haujajipanga sawa sawa, owner lazima uanguke,”alisema Kushaba.

“Tulitikisa kwakweli siwezi kukataa na inaendelea kuwa hivyo kwasababu yeye mwenyewe anakuwa hajajipanga,” aliongeza.

Kuhusu uhusiano wake na Lady Jaydee, Aneth amesema hajawahi kukutana naye japo anamchukulia kama dada yake.

“Sijawahi kukutana naye, wala kuongea naye kwahiyo sielewi chochote. Na mahusiano ya bendi na bendi pia hatujawahi kukutana kwenye stage moja nikajua kwamba tukikutana inakuwaje. Labda siku moja tukikutana ndio tutajua kwamba tuna bifu ama hatuna lakini sisi binafsi hatuna bifu na mtu yeyote.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents