Burudani

Skendo za ubakaji zazidi kumbana Mzee Bill Cosby, wanawake 15 wajitokeza

Supermodel Janice Dickinson amejitokeza kudai kuwa alishambuliwa kimapenzi na Mzee Bill Cosby.

bill-cosby-netflix-exclusive-stand-up-special (1)

Kufuatia kuongezeka kwa shutuma hizo, kituo cha runinga cha NBC, kimetangaza kufuta deal ya kufanya kipindi chake baada ya Dickinson kuwa mwanamke wa 15 anayemtupia shutuma muigizaji na mtangazaji wa kipindi mahiri cha The Cosby Show. Kipindi hicho kiliruka kuanzia 1984 hadi 1992. Cosby hajawahi kushtakiwa.

Kipindi hicho kilikuwa kifanyike mwakani ambapo Cosby alikuwa acheze kama babu kwenye familia kubwa.

“Nafanya hivi kwasababu ni kitu sahihi cha kufanua na kilitokea kwangu, na hii ni story ya kweli. Nawaamini hao wanawake wengine,” Dickinson, aliyekuwa jaji wa America’s Next Top Model kwenye mahojiano na Entertainment Tonight Jumanne.

Mi Amor Gala Havana White Party
Janice Dickinson

Anadai kuwa tukio hilo lilitokea mwaka 1982 baada ya Cosby kumwekea dawa ya usingizi kwenye chakula.

Hivi karibuni Cosby aliahirisha kutokea kwenye vipindi vya The Late Show with David Letterman na The Queen Latifah Show. Msemaji wake alisema ulikuwa ni uamuzi wake kujiondoa.

Nayo Netflix ilitangaza kuahirisha show yake ya stand up ambayo ilikuwa ikifanyike Nov. 28.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents