Habari

Siri ya ulipaji kodi wa Donald Trump yafichuka

Baada ya kuficha kwa muda mrefu, ukweli wa ulipaji kodi wa Donald Trump wafichuka. Shirika la habari la MSNBC limeripoti kuwa Rais huyo alilipa jumla ya dola milioni 38 ya kodi hiyo.

MSNBC limesema kuwa Trump alilipa kodi hiyo kutoka kwenye mapato yake ya dola milioni 150 mwaka 2015. Taarifa hiyo inaonesha Trump alilipa kodi ya $5.3m kwa serikali na kodi nyingine ya ziada ya $31m kwa kile kinachofahamika kama kodi mbadala ya chini (AMT).

Inadaiwa kuwa kodi hiyo ya dola milioni 38 ni kiwango cha 24% ya kiwango cha juu kuliko kile cha raia wa Marekani wa kipato cha kawaida. Hata hivyo ni chini ya kiwango cha 27.4% ambacho kwa kawaida hulipiwa na watu wenye kipato cha juu.

Hata hivyo maafisa wa ikulu ya Marekani wamesema ni kinyume cha sheria kuchapisha taarifa hizo.

Kwenye uchaguzi mkuu wa Urais mwaka jana mwishoni Trump aligoma kutoa taarifa hizo ambazo mgombea mwenza kutoka chama cha Democratic Hillary Clinton alimtuhumu kuwa ni mkwepaji kulipa kodi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents