Habari

Sintah kurejea TV na kipindi cha harusi


Hatimaye mtangazaji na msanii wa filamu na tamthilia nchini Christine Sintah anatarajia kurudi rasmi kwenye runinga.
Sintah anayejiita ‘mwanamke mwenye masters’ mjini atakuwa akiendesha kipindi cha sherehe za harusi kiitwacho ‘Harusini’ ambacho kitarushwa kupitia kituo cha runinga cha DTV muonekano mpya na kauli mbiu ‘Ni wakati wako’.
Kupitia website yake, Sintah amesema, “Kweli SINTAH ndani ya runinga yako ya DTV muda na saa subiria Jumapili utawekewa. Huu ndio wakati wa kukujuza kwanini nilikuwa navaa mashela kila mara, usikose Harusini na Sintah.”
September 1 mwaka huu Sintah atazindua filamu yake iitwayo ‘The Return of JLO’ ambapo waigizaji wengine waliohusika ni pamoja na Monalisa, Nyoshi El Sadaat, William Malechela na mastars wenginr.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents