Diamond Platnumz
Simu ya Diamond iliyoibiwa yasababisha kuvuja kwa ngoma yake ‘Ukimwona’
Hivi karibuni tuliweka wimbo mpya wa Diamond uitwao ‘Ukimwona’ na tukajiuliza kama kweli ameiachia rasmi ama imevuja.
Hata hivyo Diamond ameiambia blog ya Dj Fetty kuwa ngoma hiyo imevuja baada ya simu yake kuibiwa.
“Kweli kabisa siku release na hiyo nyimbo hapo ilipo haijaisha kabisa, hapa katikati nilikuwa na simu yangu blackberry bold 4 niliipoteza bahati mbaya ikaibiwa,” alisema Diamond.
“Ila kila kitu kinachotokea kwangu sometimes namshukuru Mungu kwasababu yeye ndio anaandika, watu wanaipeda sana napoenda kwenye show zangu watu wanataka niimbe, namshukuru sana Mungu.”