Michezo

Simba SC yamtangaza mchezaji wake bora wa mwezi Disemba

Klabu ya soka ya Simba SC imemtangaza mchezaji bora wa mwezi Disemba katika timu hiyo.

Mchezaji aliyefanikiwa kushinda tuzo hiyo katika kikosi hicho ni beki Method Mwanjali ambaye ni raia wa Zimbabwe ambaye pia aliwahi kuichezea Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Hivi karibuni mchezaji huyo amekuwa katika kiwango kizuri ikiwa ni siku chache zimepita tangu alipotangazwa kuwa Mchezaji bora wa mashindano katika mashindano ya kombe la Mapinduzi yaliyomalizika Januari 13 huko visiwani Zanzibar kwa Azam FC kuibuka mabingwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents