Michezo

Simba SC wafuata njia ya Yanga kuikataa Mamelodi Sundown

Klabu ya soka ya Simba SC nayo imeungana na wapinzani wao Yanga kukataa kucheza mechi ya kirafiki na mabingwa wa Afrika Mamelodi Sundown kutoka Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa mmoja wa viongozi wa Simba, amekiambia kipindi cha Sports HQ cha EFM, hawatacheza mechi hiyo katikati ya wiki hii na mabingwa hao kutokana na kubanwa na ratiba za ligi kuu ya Tanzania Bara.

Naye mratibu wa ziara ya mabingwa hao hapa nchini, Rahim Zamunda amesema wamepanga timu hiyo ya Mamelodi kuanza kucheza mechi ya kwanza na Azam FC Jumatano hii na alikuwa haoni sababu ya timu za Simba na Yanga kukataa bahati hiyo kwa kuwa hata Barcelona wiki chache zilizopita ilikuwa nchini Qatar wakati ligi yao bado inaendelea.

Mamelodi Sundown walikuja nchini kwa ajili ya ziara ya kupinga mauaji ya tembo ambapo walipangiwa kucheza na timu za Yanga, Simba na Azam FC.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents