Burudani

Sijawahi kufikiria ‘kudate’ na wasanii – Dayna Nyange

Msanii wa muziki Dayna Nyange amesema hawezi kutoka kimapenzi na wasanii wa bongo kutokana na kuwa na wivu.

Dyna Nyange

Muimbaji huyo ambaye pia ni mama wa mtoto mmoja aitwae ‘Rahma’, amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM kuwa, hapendi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mastaa kwa sababu wengi wana mambo mengi.

“Sijawahi kufikiria ‘kudate’ na wasanii kwa sababu nawaogopa, ni pasua kichwa. Mimi nina wivu sana mazingira ambayo tuko nayo nadhani nitakonda mara mia” alisema Dayna Nyange.

Dayna Nyange ni mmoja kati ya wasanii wa kike ambao hawapendi kuweka wazi mahusiano yao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents