Burudani

Sijasanda kuichana serikali, ila tu mimi si mtu wa kutabirika – Roma

Roma amekanusha madai ya mashabiki wa muziki kuwa ameufyata mkia na kuacha kuichana serikali kwenye nyimbo zake kama zamani kutokana na serikali ya awamu ya tano kuto’entertain’ mambo hayo!

Rapper huyo amedai kuwa muziki anaofanya sasa hautabiriki na ataendelea kuwashtukiza mashabiki kwa nyimbo wasizotarajia kutoka kwake.

Kwenye mahojiano na kipindi cha Extra Fleva cha Uplands Fm, Roma amedai kuwa si mara ya kwanza mashabiki kusema ameufyata. “2012 ile ndio ilikuwa noma, kwasababu ndio nakumbuka ndio nilikuwa nimeachia Mathematics halafu tukachukua tuzo mbili halafu nikakaa kimya mwaka na miezi nane,” amesema.

“Ndani ya kipindi hicho zilitokea sana kuliko hata zinazotokea sasa hivi ‘yaani huyu Roma ndio hawezi kufanya chochote, ameshapewa hela, Roma ametishiwa, Roma amepelekwa polisi, Roma amepelekwa ikulu’ yaani ziliongelewa sana halafu siku isiyokuwa na jina wakasikia 2030 watu wakasahau yote waliyoyasema,” ameongeza.

“Baada ya mwaka mambo yote yakapita wakasahau, wakarudia tena kuongea, siku isiyokuwa na jina wakaja wakasikia Viva Roma.”

Kazi za hivi karibuni za Roma zimeonekana kuwa na mrengo tofauti ukilinganisha na zile alizokuwa akizitoa miaka ya nyuma. Kwa sasa nyimbo zake zinazofanya vizuri ni Usimsahau Mchizi akiwa na Moni Central Zone na K aliyoshirikiana na Baghdad.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents