Burudani

Sifanyi muziki kwa kurelax kama watu wanavyodai – Jaffarai

Msanii mkongwe wa muziki, Jaffarai, amesema ukimya wake kwenye muziki umesababishwa na mabadiliko ya muziki na siyo kwamba anafanya muziki wa kuralax kama watu wanavyodai.

Jaffarai

Akizungumza na Bongo5 Jumatato hii, Jaffarai amesema game la muziki limewafanya wasanii wajipange sana wakati wa kutoa ngoma.

“Mimi sifanyi muziki kwa relax, ngoma zipo kama kawaida sema kipindi hichi siwezi toa ngoma alafu isiende, kwa hiyo lazima nijipange,video kali, sitaki kuachia ngoma alafu isifanye poa, mimi ni mkongwe kuna wadogo wanatuangalia sisi,”

Aliongeza,“Muziki ndio umenipa nguvu ya kufanya biashara, muziki kwangu ndio kila kitu, kwa hiyo nipo naendelea kurekodi, hata kwenye mikusanyiko sihudhurii, naogopa hizi habari broo kimya sana vipi?,”

Rappa huyo amesema bado anaendelea na ratiba yake na kuachia ngoma moja kwa mwaka, kwa hiyo mashabiki wake wakae mkao wa kula kwa ajili ya kazi mpya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents