Burudani

Shule ya muziki aliyoahidi Tunda Man kuianzisha yamtoa jasho ‘nilidhani rahisi’

Muimbaji wa ‘Msambinungwa’ Tunda Man amesema amekutana na kigingi kizito katika mpango wake wa kufungua shule ya muziki.

Tundaman

Tunda ameiambia Bongo5 kuwa alidhani itakuwa rahisi kukamilisha wazo lake hilo.

“Kuna vitu niliambiwa nivitime kwanza halafu ndo nifanye hivyo,” amesema. “Kwahiyo nimeambiwa nikamilishe vigezo ndo kibali nitapewa, kwa sababu hii ni shule kama shule nyingine. Kwahiyo tupo kwenye kukamilisha hivyo vigezo na kuna watu ninashirikiana nao kwa sababu wao wana elimu ya kutosha kwenda kulipia TRA na kuna vingine viko deep sana.”

“Mimi nilijua ni suala rahisi kumbe kuna vitu vingi ninatakiwa kuvikamilisha kitaaluma zaidi na sio kimuziki. Shule itafunguliwa mwaka huu. Nadhani kabla ya pasaka kila kitu kitakuwa tayari na wanafunzi wataanza kuingia na kujifunza.”

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents