Michezo

Shitaka la kutumia dawa za kulevya: Manji apata dhamana

Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji ameachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni 10. Manji alipandishwa kizimbani leo kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa shtaka la kutumia dawa za kulevya.

Manji amedhaminiwa na Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa. Kabla ya hapo mfanyabiashara huyo alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya Muhimbili kutokana na matatizo ya moyo yaliyompata baada ya kushikiliwa kwenye kituo kikuu cha polisi Central.

Kocha wa zamani wa Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa ambaye ni katibu mkuu wa Yanga amemdhamini Mwenyekiti ya Yanga, Yusuf Manji kwa shilingi milioni 10

Kwenye kesi hiyo Manji anashutumiwa kutumia dawa za kulevya aina ya heroin kutokana na vipimo toka kwa Mkemia Mkuu wa serikali. Mshtakiwa amekana kosa hilo.

Makamu mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga akiwa mahamakani Kisutu Dar leo ambapo Yusuf Manji amepandishwa kizimbani
Mwanasheria wa Yusuf Manji, Alex Mgongolwa akiwa kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar leo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents