Michezo

Shirikisho la soka Barani Ulaya UEFA yamsimamisha Mamadou Sakho

Shirikisho la soka Barani Ulaya UEFA,limetangaza kumsimamisha kwa siku 30 beki wa Klabu ya Liverpool Mamadou Sakho kwa ajili ya kuanza uchunguzi juu mchezaji huyo ambaye amegundulika kutumia madawa ambayo hayaruhusiwi michezoni.

337AEBD200000578-0-image-a-19_1461847071857

Kitengo cha nidhamu na maadili cha shirikisho hilo kinataraji kuanza uchunguzi huo na baadaye kutangaza matokeo yake na adhabu.

Baada ya ushindi dhidi ya Manchester United Machi 17 katika Europa Ligi, Sakho,26, alipimwa na kuonekana kutumia madawa (Fat Burner) ambayo hayarusiwi katika michezo.

Raia huyo wa Ufaransa na kilabu yake walikubaliana kwamba hatoshiriki katika mechi yoyote hadi pale Uefa itakapokamilisha uchunguzi wake

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents