Burudani

Shetta: Sina tatizo na Hemedy, itakuwa alinielewa vibaya

Msanii wa muziki Shetta amesema hana tatizo lolote na Hemedy PHD, huku akidai kuwa huenda kauli yake aliyosema kwa sasa hatafanya collabo na wasanii wa ndani tena ilinukuliwa vibaya na huenda ndo imemsababishia matatizo hayo.

shettaa

Hemedy PHD hivi karibuni baada ya kusikia kauli ya msanii huyo alitweet kuonyesha hakupendezwa na kauli hiyo.

Akizungumza na bongo5 leo, Shetta amesema kuwa kauli hiyo iliwakilishwa vibaya na vyombo vya habari.

“Nilichokisema katika project yangu mpya itakayo sitafanya collabo tena na msanii yoyote wa ndani kwa upande wangu ila kama kuna mtu anataka kufanya collabo na mimi milango ipo wazi, napenda kuweka wazi hili,nimeshafanya nyimbo sita nikiwa nimewashirikisha wasanii wa ndani, sasa huu ni wakati wa kutanua wigo kwa upande wangu, mimi binafsi sina tatizo na Hemedy, mimi nafikiri alinielewa vibaya tu, uwakilishaji wa habari katika vyombo vya habari waliwakilisha vibaya. Nitafanya collabo na mtu yeyote atakayehitaji kufanya na mimi kwenye project yake, lakini kwa wimbo nitakaotoa mimi either nifanye mwenyewe au nifanye collabo na msanii wa nje,” alisema Shetta.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents