Burudani

Shetta: Naifurahia sana ndoa yangu ya zaidi ya miaka miwili

Shetta na mke wake Leila wametimiza zaidi ya miaka miwili kwenye ndoa yao na rapper huyo amedai kuwa ni furaha tu ndio iliyotawala familia yake.

10919586_774325442655896_866572755_n

Shetta na Leila walifunga ndoa mwaka 2012 na hadi sasa wamebarikiwa mtoto mmoja wa kike aitwaye Qayllah.

Rapper huyo ameiambia Bongo5 kuwa anamshukuru Mungu kwa kumpa nguvu huku familia yake ikiwa ni yenye upendo na amani.

“Mimi nilioa huko nyuma na matunda yake ndo haya unayaona, Qayllah. Nilioa lakini sikufanya sherehe, ilikuwa kimya kimya saa kumi na mbili baada ya watu kumaliza ile swala ya saa 11 ndo ikapita. Kwahiyo Mama Qayllah ni mke wangu wa ndoa. Sikupiga picha wala nini.

10890835_1507224862873333_460041553_n
Qayllah

“Watu wengi hawakufahamu kwa sababu haikuwa na shamra shamra pia sikupenda kuweka wazi mambo yangu ya kifamilia kwa wakati huo. Lakini namshukuru Mungu mpaka sasa hivi nafurahia maisha yangu pamoja na familia yangu,” aliongeza Shetta.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents