Burudani

Shetta aelezea sababu ya kufanya video ya ‘Kerewa’ na director wa Afrika Kusini Godfather

Msanii wa muziki, Shetta ametoa sababu ya kufanya video ya ‘Kerewa’ na director Godfather wa Afrika Kusini, ambapo amedai itagharimu zaidi ya milioni 21
maxresdefault

“Godfather kafanya nyimbo kama Do me ya P square ,ameshoot Gobe ya Davido , video kibao ,wasanii wengi wa Afrika , tunaangalia kitu kizuri ,tunaangalia soko lingine la Afrika, sehemu yetu ya Tanzania kunasehemu nzuri za kufanya video lakini ma ,director wakubwa ambao wanaweza wakatufikisha mbali muziki wetu wapo huku ‘South Africa’ nilitaka kwenda kushoot Wingereza kuna vitu vikaingiliana ,kulikuwa kuna director anaitwa Mo Musa angeifanya hiyo pia ingekuwa vizuri pia , lakini pia tumemkosa Mo Musa tumempata Godfather pia ni director mkubwa, pia na zaidi na zaidi Afrika, kwaiyo kwanini nimekuja kufanya South Africa kwasababu yeye ndiyo anapatikana kwa urahisi kuliko kumtoa huku kuja Tanzania, vitu vingi vimepungua, hela niliyompa inasababisha yeye kutafuta kila kitu huku, mimi nimekuja na nguo zangu na Diamond tumekuja kushoot, tunawakuta model,tumekuta location zipo tayari, tunakuta kila kitu kipo tayari ,kwaiyo hiyo imesababisha kuja kufanya video na Godfather , pia ni channel, channel kubwa ziko huku ,kwaiyo sizani kama wapenzi wangu, fans wangu watapenda kumuona Shetta yupo pale pale wanapenda kumuona Shetta anasogea zaidi, kwaiyo hii nahisi ni fursa tosha kuja kufanya video huku na kupata channel nyingine ,wasishange tena Shetta wakimuona anafanya kazi huku na huku, kwa sababu ndiyo tumeanza hivyo. Jamaa afanyi video chini ya dola eflu 10,000 ambayo ni sawa na milioni 16 hapo ujatoa tiketi, ujatoa hotel, chakula, yani vitu vingi so inaweza ikafika katika hela ya Tanzania milioni 20 au 25” Shetta aliiambia amplifaya ya Clouds Fm

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents