Burudani

Sheria ya makosa ya mtandaoni: Bonta adai serikali imekurupuka

Serikali imekurupuka kuipitisha sheria ya makosa ya mtandaoni kwa mujibu wa rapper Bonta Maarifa.

11875593_441705909365639_1431171472_n

Akizungumza na 255 ya XXL jana, Bonta alisema licha ya kuanza kutumika kwa sheria hiyo toka September 1, bado watu wanaendelea kufanya mambo yale yale.

“Kuna msemo watu wanasema mazoea ni kilema. Mtu kubadilisha tabia ni sawa sawa na mtu kubadilisha ngozi yake. Mbaya zaidi hii sheria imekuja kipindi kibaya sana. Kipindi ambacho mambo mengi ya siasa yanaendelea, kupingana hapa na pale kwa maneno makali ndio maana unaona sheria imeanza,” alisema Bonta.

“Lakini kama hakuna sheria, majibizano ya maneno makali ndani ya mitandao bado yanendelea. Inakuwa kama hakuna sheria na mbaya zaidi kitu ninachokiona kama ni watu kushtakiwa wangetoa muda kwanza mpaka sheria kuanza. Watu waelimishwe vizuri ili taarifa zifike kwa watu wote. Mimi mwenyewe nimesikia mwezi mmoja uliopita. Mimi nipo kwenye access je wasio kwenye access si ndio shida kabisa,” aliongeza rapper huyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents