Siasa

Sheikh Yahya azushiwa kifo

Sheikh Yahya azushiwa kifo
Mnajibu maarufu Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein, amezushiwa kufariki dunia jana akiwa nchini Dubai.

Uvumi huo ulienezwa mitaa mbalimbali jijini Dar es Salaam, hatimaye
kuvifikia vyombo vya habari ikiwamo Tanzania Daima iliyokwenda
kuthibitisha taarifa hizo nyumbani kwa sheikh huyo, Magomeni Mikumi,
Dar es Salaam.

Ilielezwa kuwa Sheikh Yahya alifariki dunia ndani ya ndege iliyodaiwa
kupitia nchini Dubai, kuelekea India alikokwenda kupata matibabu.

Hata hivyo, juhudi za Tanzania Daima kutaka kupata ukweli kufuatia uvumi huo zilibaini kuwa Sheikh Yahya ni mzima.

Tanzania Daima ilipofika nyumbani kwa mtabiri huyo jana mchana,
haikuona dalili zozote za kuwapo msiba, na badala yake mtoto wa sheikh
huyo, aliyejitambulisha kwa jina la Hassan Yahya Hussein, alikanusha
vikali taarifa za baba yake kufariki.

Hassan akizungumza kwa kujiamini alisema: “Sheikh mzima, aliondoka hapa
jana (juzi) na ndege ya Shirika la Ndege la Kenya, kwenda mjini Mumbai,
India. Ndege hiyo ilipitia Nairobi, haikupitia Dubai kama hizo habari
za uzushi zinavyosema.

“Sheikh alifika salama na kupokelewa kwenye hospitali ya maradhi ya moyo iitwayo Jaslok, iliyoko Mumbai…”

Hassan alisema Sheikh Yahya yupo nchini India kwa ajili ya kutibiwa
maradhi ya moyo, baada ya kituo cha tiba za maradhi ya moyo nchini
(THI), chini ya uchunguzi wa Dk. Massau, kugundua kuwa ana tatizo la
kuwa na moyo mkubwa.

Alisema hospitali hiyo ya India ndiyo yenye uwezo wa kutibia tatizo la
kuwa na moyo mkubwa, ambalo liligundulika kuanza kumsumbua takribani
miezi mitatu iliyopita.

“Sheikh yupo mzima kabisaaaa, yupo chini ya uangalizi wa daktari wake,
Profesa Mehta. Yaani nimezungumza naye mchana huu, saa saba hii hii na
amenithibitishia kwamba yeye ni mzima. Tena aliye-finance (gharamia)
safari yake ya India, ni rafiki yake Bwana Kikwete (Rais Jakaya
Kikwete),” alisema Hassan.

Hassan alisema baba yake anatarajiwa kurejea nchini Aprili 5.

“Sheikh anatarajiwa kurudi hapa Aprili 5. Tiketi yake ya ndege
inaonyesha atakuwa hapa Aprili 5. Sheikh mzima,” alisisitiza Hassan.

Hata hivyo, taarifa nyingine zinaeleza kuwa Sheikh Yahya alizidiwa jana
asubuhi akiwa nchini India na kulazimika kukimbizwa hospitali ambapo
amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents