Burudani

Sheddy alivujisha wimbo wangu bila kupata baraka za wasafi – Harmonize

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva kutoka label ya Wasafi, Harmonize amesema producer Sheddy Clever alivujisha wimbo wake bila ya idhini kutoka kwa uongozi wa WCB.

harmonize2

Harmonize ambaye video yake ya ‘Bado’ inafanya vizuri kwa sasa ikiwa imeshatazamwa na viewers zaidi ya laki tisa kwenye mtandao wa youtube, amekiambia kipindi cha Bongo Kali kinachorushwa na City FM kuwa Sheddy Clever alivujisha wimbo wake wa ‘Moyo’ bila ya idhini ya WCB.

“Nashangaa kuona wimbo wangu wa ‘Moyo’ munayo, kiukweli huu wimbo niliurekodi siku nyingi sana kwa Sheddy Clecer lakini mambo yalikuwa mengi nikashindwa kuufanyia marekebisho. Baada ya muda kupita nilishangaa kusikia wimbo huo upo mtaani, nilimuuliza Sheddy alikataa kama yeye ndio ameuvujisha,” Alisema Harmonize.

Aliongeza kuwa, “Producer anapokuwa hana ngoma zinazopigwa kwenye media wala kusikika huwa anakuwa na stress nyingi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents