Burudani

Sharobaro V Wasafi

diamond_lagos

Ule ufa ambao mdogoo lakini mara nyingi, ulikuwa ukijitanua polepole kutaka kutoa mpasuko, sasa neno limeshatimia kwa mpasuko wenyewe kujitokeza na kuwa mkubwa kati ya Sharobaro na WASAFI yaani Bab Junior mmiliki wa studio ya Sharo baro na mwanamuziki wake Diamond.

Diamond anasema, ameamua kuachia ngazi  Sharobaro na kuanzisha Serikali mpya ya WASAFI, ikiwa na uongozi kama ufuatao kiti cha wazili mkuu kimekamatwa na Hemed Selemani ‘Phd’, huku umalkia wa WASAFI, ukienda kwa Linah na First lady akiwa Wema Sepetu wakati makamo wa raisi akiwa Sheta wa Dar Stamina.

Raisi aka Presedent wa WASAFI  ukiwa chini ya mzee wa kitengo mwenyewe Diamond, na akasema, atatangaza jinsi ya kujiunga na Group hilo, ambalo anaamini linaongoza kwa usafi, na vigezo vyake atavitaja lakini kwanza lazima uwe msafi.

6_hEMED
(Phd ‘ Hemed Seleman akiwa na Bab Joniur walipokuwa wakiimba jukwaa moja wimbo mmoja.)

Huko upande wa  Wasafi kwa upande wa Bab Junior aka Sharobaro President, yeye anasema halijui kundi la Wasafi, kwakuwa wasafi wote wapo Sharobaro.   Ilikuongezea kidogo alisema hivi sasa wanamikakati ya kuzunguka Tanzania nzima kuwatafuta maraisi wa mikoa ambao watawawakilisha Masharobaro katika mikoa yao, na kama haitoshi kama atajitokeza mtu anaimba vizuri basi watamchukua kwaajiri ya kurekodi bure.

lilol
(Lilo Boy, Meneja wa Masharobaro Record)

 

Meneja wa kundi hilo la Masharobaro Lilo Boy  naye alikuwa  na yake ya kuongea kwa kusema, hakuna mtu atakayeukimbia usafi harafu bado akajitangazie usafi, yaani hapa alimaanisha Usharobaro ndiyo Usmart, yaani usafi.

 

Aliongeza kwa kusema kila msanii anayeingia Sharobaro yeye ndiyo anayemsainisha mkataba, hivyo  hata huyo aliyehasi kutoka kwa masharobaro, yeye ndiye aliyemsainisha mkataba wa kuimba bule lakini sasa hivi kawa Muhasi.

KAZI KWAKO MDAU, UENDE UPANDE GANI?

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents