Michezo

Shabiki wa Leicester kushinda £25,000 iwapo itashinda taji la ligi

Shabiki mmoja mwenye mapenzi na kilabu ya Leicester huenda akajishinda pauni 25,000 iwapo timu yake katika ligi ya Uingereza itachukua taji la ligi hiyo baada ya kuweka pauni tano katika dau la 5,000-1.

160206145519_leicester_city_640x360_getty_nocredit

Baada ya ushindi wa Leicester wa 3-1 dhidi ya Manchester City unawaacha wakiwa pointi tano juu ya jedwali hilo huku ikiwa thuluthi mbili za msimu huo zimekamilika.

Carpenter Leigh Herbert, mwenye umri wa miaka 38 alicheza dau akiwa katika likizo na amekataa ombi la kumtaka achukue pauni 3,200 ili kujiondoa.

Iwapo Leicester ambao walikuwa chini ya jedwali la ligi hiyo mwaka mmoja uliopita watashinda taji hilo la ligi, basi inaaminika kuwa hiyo itakuwa zawadi kubwa kuwahi kutolewa katika historia ya michezo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents