Burudani

Shaa: Sugua Gaga imebadilisha maisha yangu ‘completely’

Sugua Gaga haijamfanya Shaa kuwa msanii wa kwanza Tanzania kuwa na video iliyoangaliwa zaidi kwenye Youtube peke yake, bali pia imebadilisha maisha yake kwa kiasi kikubwa.

10689803_10152770334968570_3455746866143959303_n

Akiongea mchana wa leo kwenye kipindi cha Mseto cha Radio Citizen ya Kenya, Shaa amesema kuwa wimbo huo umemfungulia milango mingi kuliko alivyokuwa akitarajia ikiwa ni pamoja na kuitwa kwenye kipindi cha Coke Studio Africa.

Shaa amesema hivi karibuni pia atasaini mkataba mnono na kampuni kitu ambacho kisingewezekana bila Sugua Gaga.

Amesema alichojifunza kutokana na mafanikio ya Sugua Gaga ni kuwa ni muhimu kwa msanii kuanza kufanya muziki kwa ladha ya nyumbani zaidi kabla hajaanza kufikiria kufanya muziki wenye ladha ya mataifa mengine.

Ameongeza kama msanii akifanya muziki utakaopendwa nyumbani ni rahisi sana kuhit nje ya nchi. Hata hivyo Shaa amedai kuwa kipindi anatoa wimbo huo, watu wengi walimkejeli kuwa amepotea kutokana na muziki aliokuwa amezoea kufanya.

Hata hivyo amesema mafanikio ya wimbo huo yamewafanya wasanii wengine kufuata kile alichokifanya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents