Burudani

Shaa asema amefanya Collabo na Redsan baada ya kugundua ndiye msanii anayeheshimika zaidi Kenya, AY ndiye aliyewaunganisha

Baada ya kuachia video mpya ‘Njoo’ iliyoongozwa na director Enos Olik, Shaa amezungumzia mambo kadhaa kuhusu collabo hiyo mpya na star mkubwa wa Kenya, Redsan ikiwemo sababu za kumchagua kumshirikisha pamoja na mtu aliyemsaidia kumpata Redsan kiurahisi na kufanya nae kazi.

shaa

Shaa amesema baada ya kufanya utafiti aligundua Redsan ndiye msanii anayeheshimika zaidi Kenya ambaye angeweza kumtambulisha vizuri zaidi huko.

“Nikasema nikifanya collabo na mtu wa huku ili wanielewe kidogo wanisikie zaidi , hakuna msanii anaheshimika kama Red Sun, na Katika kufanya research hakuna msanii anaeheshimika Kenya kama Redsan, hakuna babu yaani hiyo hands down, unajua mimi mwenyewe nilifikiria Nameless , nikaanza kuwataja kina Octopizzo ambao nao wana heshima zao..lakini babu nimekuja kugundua Redsan ni mziki mwingine kabisa ni noma” Alisema Shaa kupitia FNL ya EATV jana.

Redsan2

Shaa ambaye jina lake halisi ni Sarah Kaisi amesema kuwa AY ambaye aliwahi kumsimamia zamani chini ya Unity Entertainment, ndiye ambaye amewezesha zoezi zima la kumuunganisha na Redsan pamoja na kusimamia kazi yote hadi video licha ya ugumu wa kupatikana kwa msanii huyo toka asaini mkataba wa kimataifa wa kusimamiwa na Sony.

“Nimepiga interview kumi, kila mtu ananiuliza umempataje? Wanasema Redsan haonekani , ever since kasaini na Sony yuko International … Credit yote kwakweli iende kwa Ambwene Yessaya, AY Unity Entertainment ndio walisuka the whole deal, mpaka siku ya kushoot walipaa, tulikutana Kenya nikawaambia yooh nipo Kenya, akaniambia aah na mimi nipo Kenya, kama vipi Shaa si tufanye na video moja kwa moja, nikamwambia aah nikatae tena. AY ikabidi afly in, wakapanda lindege lile wakatua kina Unit Entertainment wakaja wakasimamia mzigo mzima ambao ulifanyiwa na Enos Olik director ambaye anakuja vikali sana sana in East Africa and Africa actually.”

Alimalizia kwa kusema:

“Kwahiyo hiyo ndio main reason ambayo nimemtumia Redsan kutokana na heshima yake na ni utambulisho mzuri sana kwangu mimi Kenya, hapa nyumbani hata mimi nilivyoambiwa Redsan nikasema mbona nyumbani hatumsikii na recently tu kama wiki iliyopita ametoa na yeye wimbo wake mpya…kwahiyo kwangu mimi naweza kusema ni God sent, wakati muafaka, ni mkubwa sana Kenya hapa Tanzania unajua tunamchukulia poa”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents