Videos

Shaa aachia video ya Lava Lava

Mwanamuziki wa kundi la zamani la Wakilisha, Sarah Kaisi aka Shaa, ameachia video ya wimbo wake mpya, Lava Lava. Video hiyo imefanywa na Adam Juma wa Visual Lab: Next Level.

Akiongea na Bongo5 hivi karibuni, Shaa alisema Lava Lava ni video anaiachia kwaajili ya kujidhatiti katika soko la Afrika.

“Kwa bongo hapa ilikuwa tuanze na Promise halafu nilikuwa nitoe Lava Lava kwaajili ya soko langu la nje la Africa kwasababu sijatoa wimbo mwaka jana at all so nikaona mwaka huu nikaona siyo mbaya nikitoa nice song a nice video ambayo hata Dar hapa pia nitaitoa kwa sababu ni nyumbani lakini the focus ni nje, East Africa ,West Africa, South Africa and all that,” alisema Shaa.

Katika video hii Shaa akiwa na kundi la madansa wa kike anaonesha uwezo mkubwa wa kucheza kwenye mdundo wa wimbo huo uliotengenezwa na producer Giggz katika studio za MJ Records.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents