Habari

Serikali yatangaza vita na wafanya biashara wa unga, watuhumiwa 719 wakamatwa

Serikali imesema haitakuwa na msamaha wala suluhu kwa wahusika wote wa biashara haramu ya dawa za kulevya.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga alitoa rai kwa watu wote kutojihusisha na uuzaji, utumiaji na usafirishaji wa dawa hizo.
1

Kitwanga aliyasema hayo jana bungeni mjini hapa wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake, kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Alisema, tatizo la biashara haramu na matumizi ya dawa za kulevya limeendelea kuwepo nchini na katika kipindi cha Julai, 2015 hadi Machi, 2016, kilogramu 141.7 za dawa za kulevya za viwandani ambazo ni heroin, cocaine, cannabis resin, morphine na mandrax zilikamatwa na watuhumiwa 719 (wanaume 644 na wanawake 75) walikamatwa na kufikishwa mahakamani.

“Aidha, kilo 18,513 na gramu 415 za bangi na kilo 15,402 za mirungi zilikamatwa ambapo watuhumiwa wanaume 9,935 na wanawake 1,020 walikamatwa na kufikishwa mahakamani,” alisema.

Alisema, katika mwaka 2016/17 Jeshi la Polisi litaendeleza mapambano dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya kwa kubaini mtandao wa wahalifu wa ndani na nje ya nchi unaojihusisha na uingizaji na usambazaji wa dawa za kulevya nchini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents