Habari

Serikali itaendelea kutumbua majipu – Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli amesema yeye na serikali yake itaaendela na utumbuaji wa majipu kwa wale wote viongozi walio kinyume na maadili huku akisema kuwa ni bora achukiwe na watu wachache.

Kauli hiyo ameisema mkoani Shinyanga Alhamisi hii wakati akizungumza na wananchi kuhusu maendeleo ya mkoa huo na kumbukumbu ya maadhimisho ya Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar huku akisema kuwa yeye amejitoa sadaka kwa ajili ya nchi.

“Mimi sikuwa na urais ila mmenipa nyie, sasa nawaahidi mimi na serikali yangu tutawatetea kwa nguvu zote dhidi ya mafisadi,” alisema.

“Ni bora nichukiwe na watu wachache kuliko kupendwa na wengi huku mambo yakienda mrama. Wale wote wanaodai mtindo wangu wa kutumbua ni mbaya hawa ndio majipu. Kabla ya utumbuaji watanzania walikuwa wanaishi maisha ya ajabu, huku akiweka msisitizo kuwa alikuwa mtumishi wa serikali kwa kipindi cha miaka 10 anajuani nini anachoongea,” alisema.

Aidha Rais Magufuli aliomba Watanzania wamuombee ili aweze kuendeleza jitihada zake za kupambana na mafisadi kwani serikali yake ya awamu ya tano imejipanga kuendelea kuongoza kwa ukali kwa faida ya watanzania wote wakiwemo wanyonge na maskini.

BY: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents