Bongo Movie

Serikali isipokuwa makini, miaka 3 ijayo hakutakuwa na filamu za Bongo – aonya Dr Cheni

Msanii mkongwe wa filamu nchini Dr Cheni amesema kuwa serikali isipokuwa makini baada ya miaka 2/3 kiwanda cha filamu za Tanzania kitapotea.

Dr Cheni
Dr Cheni

Akizungumza kwenye kipindi cha Mkasi TV hivi karibuni, Cheni alisema hata wauzaji wakubwa na wasambazaji wameshaanza kupata hasara kutokana watu wanaotengeneza nakala feki.

“Unajua huko tunakokwendea kama hali hii itaendelea after four years hakutakuwa na movie ya kitanzania inayouzwa,” alisema Cheni. “Kwa sababu msambazaji ananunua master kwako labda amenunua milioni thelathini, ana mashine ya kurudufu, mpaka movie yako inatoka amepoteza labda milioni 100, lengo lake arudishe kwanza milioni mia halafu atafute faida kwa sababu analipa kodi, analipia majengo.

Siku ya kwanza anaingiza movie sokoni leo, after two days movies tayari ipo mikononi mwa watu ambao ni wezi wa kazi. Hata ile movie anayotegemea kuuza hatauza tena kwa sababu watu tayari wanayo. Nani atafanya biashara namna hiyo? Ndio maana nakwambia serikali isipotilia mkazo na movie ndio ina watu wengi sana wamejiajiri inakwenda kupoteza ajira hiyo. Nataka nirudie tena serikali isipokuwa makini baada ya miaka 2/3 game la movie halitakuwepo tena,” alisisitiza Cheni

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents