Habari

Serikali ipo tayari kufuta sheria za vyombo vya habari zilizopitwa na wakati

Serikali imesema ipo tayari kushirikiana na wadau katika sekta ya habari kubadilisha baadhi ya sheria na kanuni zinazoongoza tasnia ya habari ambazo zinaonekana kubana na kukandamiza tasnia hiyo kwa kwendana na mabadiliko ya wakati na teknolojia.

Waziri wa Habari,Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametoa kauli yake wakati wa ziara yake aliyoifanya katika vyombo vya habari vya IPP yenye lengo la kuangalia changamoto ambayo sekta hii ambayo inakabiliana nazo. Waziri huyo amesema wakati umefika sasa wa kubadilisha sheria na kanuni zinazobana vyombo vya habari.

“Mimi kwa upande wangu siamini kwamba kamati ya maudhui kazi yake ni kupiga faini, kazi yao lazima itoke kwenye kupiga faini iende kwenye kuelezana. Sasa ukiwaambia watakwambia sheria, kwahiyo sheria tukashughulike nayo basi na mimi natamani kwakuwa mimi ndo ninayepeleka sheria bungeni, bahati nzuri kanuni mwisho ni kwa waziri na ukisoma hukumu nyingi wanacheza na kanuni so it’s me to change basi, na mimi huko ndo nataka twende,” alisema Nape

“Lakini nikasema nisiende kama ninavyohisi mimi niende kama mahitaji ya wadau yalivyo na ndio maana ni swali hilo tu mna kikwazo wapi tukae chini tuone kama pana uwezo wa kubadilisha tubadilishe.”

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbas amevihakikishia vyombo vya habari nchini ushirikiano mzuri katika kupata habari za serikali kutoka katika vitengo vyote vya mawasiliano serikalini

“Niwahakikishieni ndugu zangu wanahabari kuwa suala la upatikanaji wa habari kutoka serikali litakuwa si la kusumbuana tena na tunatengeneza mfumo katika vitengo vyote vya mawasiliano serikalini ili iwe rahisi kupata taarifa kutoka kwetu,” amesitiza Dk Abass.

BY: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents