Burudani

Serengeti Fiesta Dar kuonekana live mtandaoni

Waandaji wa tamasha la Serengeti Fiesta kwa kushirikiana na Clouds TV wametangaza kurusha mtandaoni moja kwa moja sehemu ya matangazo ya tamasha la Serengeti Fiesta 2014 ambalo mwaka huu litashereheshwa na mwanamuziki kutoka Marekani, T.I ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya Grammy.

Attachment-1

Tamasha hilo litafanyika katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam tarehe 18 mwezi wa kumi mwaka 2014

Kwa mujibu wa TanzaniaBox.com baadhi ya vipande vya sehemu ya tamasha la Serengeti Fiesta na matukio maalumu ya nyuma ya pazia yatarushwa moja kwa moja na yataweza kutazamwa popote pale duniani kwa kifaa chochote kilichounganishwa na mtandao wa intaneti kama simu zenye uwezo wa kuonyesha video, komputa ndogo, komputa kubwa pamoja na TV zilizounganishwa na mtandao.

Mashabiki wa Serengeti Fiesta duniani wataweza pia kufuatilia moja kwa moja pale wasanii wakubwa wa Bongo Flava kama Diamond, Ali Kiba, Ney wa Mitego na Vanessa Mdee pamoja na wasanii wengine wa kimataifa kama Waje, Victoria Kimani, Ash Hamman pamoja na mkali kutoka Marekani T.I wakitoa burudani.

TanzaniaBox.com ni televisheni mpya ya mtandaoni yenye makao yake jijini Dar es Salaam ambayo imejikita katika kusambaza maudhui yenye mlengo wa kitanzania kwa watazamaji duniani kote na mpaka sasa ina watazamaji kutoka zaidi ya nchi 70 kutoka pande tofauti za dunia ambao wanatembelea mtandao huo ili kupata taarifa muhimu kupitia muunganiko wa vituo vya TV kutoka Tanzania pamoja na kutazama vipindi vya televisheni wanavyovipenda.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents