Michezo

Serena Williams alitwaa ubingwa akiwa na ujauzito

Mchezaji nguli wa tennis namba moja kwa sasa duniani, Serena Williams amejitangaza kuwa ni mjamzito kupitia Snapchat.
A

Habari hizi zinaonyesha kwamba, Serena alikua Mjamzito wa wiki nane, pale alipotwaa ubingwa wa Tennis katika Mashindano ya Australian Open, jijini Melbourne mnamo January mwaka huu.

Mwanadada huyo mwenye miaka 35 aliweka picha yake akiwa amejipiga picha kwenye kioo na kuandika 20 weeks yaani, majuma 20 kisha akaifuta hiyo post.

Iwapo itathibitika kwa hakika kuwa ni mjamzito, Serena anaweza kuzikosa Grand Slams tatu mwaka huu, zikiwemo French Open, Wimbledon na US Open.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents