Habari

Sean Kingston amalizana na msichana aliyemtuhumu kumbaka (gang rape), kwa kumlipa pesa

Baada ya msanii wa Marekani mwenye asili ya Jamaica Sean Kingston na mlinzi wake kutuhumiwa kumbaka msichana mmoja mwaka 2010 kwa kumchangia (gang rape), Staa huyo ameamua kuimaliza kesi hiyo kwa kumlipa mlalamikaji kiasi cha pesa kama alivyohitaji.

sean k

Vyanzo vimeuambia mtandao wa TMZ kuwa Sean si kwamba amefanya hivyo kwa sababu amekubali kosa, lakini ameamua kumaliza matatizo ili kesi hiyo iishe sababu anategemea kuanza kufanya ziara ya muziki pamoja na kutoa album mpya hivyo hatapata muda wa kutosha kufatilia mambo ya kesi.

Vyanzo hivyo vimeendelea kusema kuwa Kingston amemlipa msichana huyo pesa lakini haijajulikana ni kiasi gani. Msichana huyo aitwaye Carissa Capeloto (22) alidai kuwa kutokana na tukio alilofanyiwa kumletea matatizo katika maisha yake alidai mwimbaji huyo amlipe kiasi kisichopungua dola za Marekani milion 5.

Chanzo kimoja kimesema hata kama Sean angeendelea na kesi hiyo bado ameshinda tu sababu msichana huyo alikuwa anatoa maelezo yanayojikanganya kila alipokuwa akihojiwa na maaskari , na pia rafiki yake na msichana huyo pia alitoa maelezo yanayotofautiana na ya Capeloto na kuwa ripoti ya hospitali haioneshi dalili zozote za kulazimishwa kufanya mapenzi (kubakwa) kama alivyodai.

Kama ilivyoripotiwa awali, Sean Kingston alikili kufanya mapenzi na msichana huyo aliyekuwa na miaka 19 wakati huo (2010) lakini kwa makubaliano. Kesi hiyo inategemewa kufutwa muda si mrefu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents