Burudani

Sauti Sol washindwa kuendelea hatua ya mwisho kuwania ‘Worldwide Act’ ya MTV EMA

Washindi wa MTV EMA ‘Best African Act’ na waliokuwa wawakilishi pekee wa bara la Afrika katika kipengele cha ‘Worldwide Act’ kwenye tuzo za MTV EMA, Sauti Sol kutoka Kenya hawajafanikiwa kuvuka mchujo wa ngazi ya kanda kuendelea kwenye hatua ya mwisho ya kumpata mshindi.

sauti-sol1

MTV EMA jana Oct 30 imetangaza majina ya wasanii 10 waliofanikiwa kufika hatua ya pili na ya mwisho ambayo itatoa mshindi wa kipengele hicho.

Mohammed Assaf, muimbaji kutoka Palestina ndiye amewashinda Sauti Sol (Afrika) na Yo Yo Honey Singh (India) waliokuwa wakiwania kuwakilisha Africa, India, Middle East.

Wasanii wote 286 walioingia hatua ya kwanza walipigiwa kura na mchujo kufanyika na kubaki majina 10.
Mshindi wa ‘Worldwide Act’ atatangazwa Jumapili ya November 9.

Hawa ndio 2014 MTV EMA Worldwide Act nominees:

Africa, India, Middle East – Mohammed Assaf
Australia, New Zealand – 5 Seconds of Summer
Europe Central – Revolverheld
Europe East – Dawid Kwiatkowski
Europe North – One Direction
Europe South – Alessandra Amoroso
Japan, Korea – B.A.P
Latin America – Dulce Maria
North America – Fifth Harmony
SE Asia, Mainland China & Hong Kong, Taiwan – Bibi Zhou

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents