Burudani

Sauti Sol waibuka ‘Best African Act’ wa MTV EMA, sasa kuwania ‘Worldwide Act’

Kundi la Sauti Sol la Kenya limewabwaga Diamond, Davido na wasanii wengine wawili wa Afrika katika kipengele cha ‘Best African Act’ cha tuzo za MTV EMA.

10636045_10153034983512262_6562077889966260389_n

Hata hivyo huo sio mwisho kwakuwa Sauti Sol sasa watahitaji kura za bara zima la Afrika kuwania kipengele cha ‘Worldwide Act’ Kuanzia leo, October 23, hadi 29 October wasanii waliovuka kwenye ngazi ya kanda wataingia kwenye hatua ya pili ya kuwania kipengele hicho kinachowaniwa na kanda za Africa/India/Middle East

Msanii mwenye kura nyingi katika vipengele hivi vya kanda atakuwa nominee wa kanda hiyo. Hadi sasa wanaowania kipengele hicho ni:

Sauti Sol (Africa)
Yo Yo Honey Singh (India)
Mohammed Assaf (Middle East)

Ingia hapa kuwapigia kura Sauti Sol.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents