Kama sio DStv potezea
TECNO Spark 2

Michezo

Samatta apata changamoto mpya ndani ya KRC Genk

By  | 

Klabu ya KRC Genk baada ya kuumia mshambuliaji wao Nikolaos Karelis ambaye alikuwa anashindania namba na mtanzania Mbwana Samatta atangazwe kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi 8 hadi 9 baada ya kupata jeraha la goti la kushoto alilolipata wakati wa mchezo dhidi ya KAA Gent December 27.

Katika kipindi hiki cha usajili January 10 2017 klabu ya KRC Genk imetangaza kufanya usajili wa mshambuliaji Jose Naranjo kutokea Celta Vigo ya Hispania, mchezaji huyo anakuja kumpa changamoto mpya Mtanzania Mbwana Samatta kuendelea kupambania namba ya kucheza na Naranjo katika kipindi ambacho Karelis atakuwa nje.


Mshambuliaji Nikolaos Karelis ambaye kwasasa ni majeruhi

Mchezaji Jose Naranjo amesajiliwa kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu wakuitumikia klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji akitokea Celta Vigo ya Hispania. Naranjo ambaye ana umri wa miaka 22.


Mchezaji Jose Naranjo ambaye amesajili na KRC Genk

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments

Bongo5

FREE
VIEW