Michezo

Salomon Kalou: Nafikiria kuachana na soka la kimataifa

Mchezaji Salomon Kalou mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast amesema anaona kuna umuhimu wa kuachana na soka la ngazi ya kimataifa.

kalou-Salomon

Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea ameichezea nchi yake michezo 81 na kufunga mabao 29. Akizungumza na Bbc kalou amesema” nimeshinda kombe la afrika nimecheza fainali mbili za kombe la dunia .Lakini nafikiri ni muda sahihi wa kuacha soka la timu ya taifa.”

“Nitafikisha miaka 30 mwaka huu na ninaanza kufikiria kuhusu kuupumzisha mwili wangu .”

Kalou ameongeza kwa kusema anahisi ni wakati sahihi kuelekeza nguvu zake kwenye klabu yake ya Hertha Berlin. Mshambuliaji huyu alijiunga na Hertha Berlin mwaka 2014 na kufunga jumla ya magoli sita katika msimu wake wa kwanza

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents