Burudani

Salma Apewa taji la utalii Tanzania

 

Bodi ya Utalii nchini Tanzania TTB jana imemkabidhi zawadi ya Domestic Tourism 2010 kwa Salma Mwakalukwa akiwa mshindi wa taji hilo katika shindano la Miss tz 2010, kwa kukidhi  vigezo vilivyowekwa.

Mkurugenzi mtendaji wa wa TTB Dr. Aloyce Nzuki alikumkabidhi rasmi Balozi huyo ndani ya ukumbi  ya bodi ya Utalii jijini Dar es Salaam kwa  kukuza Utalii wa ndani , ilkiwa amemkabidhiwa zawadi ya computa ndongo aina ya Dell   yenye thamani ya shilingi 1,100,000 na hundi yenye thamani ya 2,900,000

Aloyce Nzuki alisema kuwa sehemu ya fedha  zilizotolewa zilitumika  kwa kugharamia safari ya walimbwende wote 30 na  kutembelea Hifadhi za Serengeti, Manyara, Bonde la Ngorongoro na kwenye mapango ya Amboni Tanga.
Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii iliandaa semina kwa walimbwende hao kuhusu utalii wa ndani pamoja na shindano la kumtafuta Balozi wa Utalii wa Ndani 2010 hivyo basi wakafanya  semina na uchaguzi wa Balozi wa Utalii wa ndani ilifaifanyika tarehe 06/09/2010 katika hoteli ya Giraffe iliyopo jijini Dar es Salaam.

Awali aliongezea kuwa katika semina hii mada mbalimbali zilitolewa juu ya maana ya utalii/utalii wa ndani, taasisi zinazosimamia sekta ya utalii nchini, aina za utalii/watalii, faida za utalii/utalii wa ndani na vivutio mbalimbali vilivyopo hapa nchini, ambapo mwakilishi wa TTB alizungumzia, pamoja na mambo mengine, majukumu ya TTB, mbinu za utangazaji utalii/utalii wa ndani na changamoto zilizopo katika kukuza utalii wa ndani nchini. Pamoja na semina hii walimbwende walipewa majarida yanayoelezea utalii wetu.

Wakati wakitoa mada hizi, walimbendwe waliuliza na kujibu maswali yaliyodhihirisha upeo wa juu wa masuala ya utalii wa ndani nchini. Mambo yaliyojitokeza kwenye majadiliano haya ni pamoja na umuhimu wa kuimarisha miuondombinu, juhudi za TANAPA na NCAA kuhifadhi na kukuza utalii, changamoto za kifedha kwa wananchi na umuhimu kutangaza utalii kwa wananchi wengi zaidi

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents