Burudani

Sallam aeleza majukumu yake kama meneja wa Diamond

Mmoja kati ya mameneja wa Diamond Platnumz, Sallam ameeleza majukumu yake akiwa kama meneja wa msanii huyo ambaye kwa sasa ana mafanikio makubwa ya kimuziki Afrika.

11325904_975175485850122_1433277822_n

Akizungumza na Swahili Talk Radio ya nchini Denmark, Sallam alisema ingawa wote wamegawana majukumu lakini pia wanashirikiana katika maamuzi ya kila jambo.

“Hapa kuna meneja, kuna business meneja yaani wote tunashirikiana katika kila suala ambalo linaletwa kama ajenda ‘jamani mwaka huu 2016 tunafanyaje’ labda ajenda zipo 15, tunatakiwa tufanye tour, nyimbo tutoe ngapi na target yetu ni hii, goal yetu ni hii. Kwahiyo ni vitu ambavyo vyote vinawekwa juu ya meza na tunajadili,” alisema.

Msikilize zaidi hapo chini.

https://soundcloud.com/swahili-talk-radio/sallam-platnamz-meneja-interview-1

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents