Habari

Saida karoli asema umaarufu alioupata kwenye muziki haulingani na kipato chake

Muimbaji wa muziki wa asili nchini Saida Karoli amefunguka kwa kusema ingawa alikuwa ni mmoja ya wasanii wakubwa hapa nchini hakuweza kunufaika kutokana na kampuni iliyokuwa ikimsimamia katika muziki wake kumlipa ujira mdogo.

saida

Saida ambaye aliwahi kutamba na nyimbo kibao ukiwemo Maria Salome na Mapenzi Kizunguzungu ameliambia gazeti la Mwanaspoti kuwa umaarufu aliokuwa nao haukufanana na kile alichokitia mfukoni mwake.

“Siwezi kuweka wazi mshahara niliolipwa ila nakumbuka nilifanya shoo za kulipwa kwa dola na kuzunguka nchi mbalimbali duniani ila nililipwa kwa fedha ya Kitanzania tena mshahara uleule kila mwezi, nashukuru kwa sasa ninajisimamia mwenyewe ninapata fedha nyingi sana ingawa sina jina kama zamani” alisema Saida.

Kwa sasa msanii huyo ameweka makazi yake jijini Mwanza na wimbo wake wa sasa unaitwa Mashamsham kutoka kwenye album yake ya Pesa Inawasha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents