Burudani

Said Fella: Mwaka 2040 au 2060 kama ntakuwepo naweza kuja kuwa Rais wa nchi hii

Said Fella ana ndoto kubwa katika career yake ya siasa. Si tu kwamba anataka aje kuwa mbunge siku za usoni, Fella ana ndoto ya kuwa mkuu wa nchi kabisa.

Meneja huyo mkongwe katika tasnia ya muziki wa Bongo Fleva na aliyejitengenezea umaarufu mkubwa kupitia kundi la TMK Wanaume Family kwa sasa ni Diwani wa kata ya Kilungule jijini Dar es Salaam. “Kuna watu walikuwa wananiona huyu si mbongo flava tu huyu?, lakini wengi wameanza kuuliza kwanini usichukue ubunge?” Fela amemuambia mtangazaji wa Ice Fm, Gami Dee.

Alipoulizwa kama ana ndoto za kuja kugombea ubunge hapo baadaye Fela amesema, “Sio ubunge tu Mwenyezi Mungu akinijaalia uhai na miaka ikiwa mingi 2040 huko kama ntakuepo 2060 naweza kuwa kiongozi wa nchi hii,” alisema.

Na pia alipoulizwa kama anataka kuwa Rais, Fela amesema “enheee, ishi kwa malengo bwana.”

Hata hivyo changamoto kubwa anayokumbana nayo Meneja huyo anasema analea vijana wengi na wazazi wa vijana wanajitenga na watoto wao hawajui wanakula nini, wanalala vipi. Amesema lakini watoto wao wakitoka tu kimuziki hapo ndipo ndugu hujitokeza kwa maneno ya ajabu.

Pia amewaomba Watanzania kumsapoti Chege na wimbo wake wa ‘Kelele za Chura’ aliomshirikisha Nandy na kuahidi mazuri mengi kutoka kwa Mkubwa na Wanawe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents