Burudani

Said Fella: Bila kuwekeza fedha kwenye muziki msanii unapoteza tu muda

Mwanzilishi wa kundi la muziki Wanaume Family na Yamoto Band, Said Fella amesema kama msanii anataka kufanya muziki, lazima yeye au uongozi unaomsimamia wawekeze fedha kwenye muziki wake.

fella3

Fella amewataka wasanii kuacha kuupeleka muziki wao kishkaji shkaji na waonyeshe nia ya dhati kwenye muziki wao.

“Kila msanii ana malengo na muziki anaoufanya, ukiamua kuwa mwanamuziki kampuni lazima utie pesa’, yaani uamue kabisa ngoja nifanye muziki fulani. Maana ya pesa sio lazima uwe na milioni kumi, milioni ishirini. Ni useme ‘mimi sitaki mwana Marco Chali anitengenezee beat bure au Adam Juma anifanyie video bure kishkaji shikaji tu. Yaani Adam Juma akisema milioni nne mpe milioni nne akufanyie kazi yako. Marco Chali akisema beat laki tano mpe laki tano yake afanye kazi yake. Mpaka hapo ndo tutakuwa tumejiweza kufanya biashara ya muziki, kufanya muziki ule wa kampuni,” amesema Fella.

“Kikubwa kila msanii anatakiwa kuwa na nia na achokifanya,” ameongeza. “Kwa sababu mwisho wa siku kila msanii anatakiwa kutambua anafanya muziki gani? Huu muziki ninaofanya ni wa biashara au la? Au muziki wa maendeleo. Ukifanya muziki wa kikampuni ina maana sitaki tena nidondoke. Kwahiyo lazima utakuwa unatengeneza muziki wako pamoja na maisha yako.”

“Lakini kuna watu wengine wanafanya muziki lakini hawana malengo kama hayo niliyoyasema, wana malengo mengine wanayoyafikiria. Wengine wanasema nikipata pesa ninunue gani, wengine ninunue nyumba kila mmoja ana malengo yake. Kwahiyo lazima ujitambue muziki gani unataka kufanya.

Hata mimi sikumwambia Master Jay kwamba muziki anaoufanya Shaa ni mbaya, ila nilimwambia kuna muziki akifanya Shaa mafanikio yatakuwepo, kwamba huyu anafanya ndiyo lakini wanasikiliza matajiri lakini tajiri atasikiliza muziki wakati yupo kwenye gari, atasikiliza muziki kama ataenda kwenye kumbi za starehe. Lakini akiwa ofisini kwake ataangalia muziki wa Ulaya tu, hafikirii muda wote kwamba atasikiliza muziki wa fulani. Lakini kuna watu wanasikiliza muziki huo muda wote na ndo kama maisha yao. Ndio maana Shaa akaamua kufanya muziki unaopendwa na watu wengi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents