Michezo

Sahau kuhusu Messi, hivi ndivyo Jordi Mboulo alivyowafanya watoto wa Dortmund kwenye Uefa (Video)

Wakati ukiwa unamfahamu Lionel Messi wa kikosi cha timu ya wakubwa ya Barcelona hutakiwi kusahau kwenye klabu hiyo katika timu yao ya vijana chini ya umri wa miaka 19 kuna kinda anaitwa Jordi Mboula ambaye anadaiwa kuwa Messi mpya katika timu hiyo.

Wakati timu hiyo ya wakubwa ikiwa na mlima mrefu wa kuupanda katika michuano ya kombe la mabingwa barani Ulaya baada ya kufungwa magoli 4-0 na PSG wiki iliyopita, Mboula Jumatano hii alifanikiwa kuiongoza timu ya vijana ya Barcelona katika mashindano kama hayo lakini ya vijana kuifunga Borussia Dortmund 4-1 wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani.

Mboula ambaye ana miaka 17 amezaliwa Hispania lakini pia ni raia wa Congo DRC alifanikiwa kufunga goli moja kati ya hayo manne lakini kubwa zaidi watu wameanza kumfananisha na Messi kutokana na alivyoonyesha uwezo wake mkubwa mpaka kupatikana kwa goli hilo.

Magoli ya vijana hao yalifungwa na Carlos Perez, Abel Ruiz, Seungwoo Lee na Mboulo. Mwanzoni mwa msimu huu mchezaji huyo pia aliingizwa kwenye kikosi B cha Barcelona.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents