Burudani

Sababu za ugomvi baina ya mapacha wa P-Square zafahamika (details)

Taarifa juu ya ugomvi ulioibuka wiki iliyopita baina ya ndugu mapacha wa kundi la P-Square Peter na Paul na kaka zao zimewashtua mashabiki wao walioko pande mbalimbali za dunia. Chanzo kimoja cha karibu na ndugu hao kimeelezea sababu na kile kilichotokea.

okoye

Inadaiwa kuwa ugomvi wa wanandugu wa familia ya Okoye ulianzia kwa wasaidizi wao binafsi, ‘Personal Assistants’ (PA’s).

Ripoti kutoka katika vyanzo mbalimbali vya Nigeria zinasema kuwa ‘PA’ wa kaka yao mkubwa Jude aitwaye Wande alimpatia ‘PA’ wa Peter aitwaye Shege, pesa ili akamsajilie gari lake, lakini inasemekana ‘PA’ wa Peter badala ya kutumia pesa hizo kwa kazi aliyoelekezwa alizitumia kwa kitu tofauti.

Baada ya hapo inadaiwa kuwa ‘PA’ wa Jude alikasirika baada ya kugundua kuwa pesa alizompa ‘PA’ wa Peter hazikufanyiwa kazi aliyoelekeza. Alipoenda nyumbani kwa Okoye’s ‘Squareville’ ili kukabiliana na ‘PA’ wa Peter ndipo ugomvi ulizuka baina ya wasaidizi hao wawili wa ndugu.

Chanzo kinaendelea kusema baada ya ugomvi kuanza Peter aliingilia na kutaka kumpiga msaidizi wa Jude hadi Paul alipoingilia kwa lengo la kuwaachanisha, lakini badala yake Peter alijikuta akimpiga ngumi pacha wake Paul na kuanguka chini japo inadaiwa kuwa Paul hakumrudishia ngumi kaka yake, na badala yake kaka yao mwingine aitwaye Tony naye aliingilia na kuanza kupigana na Peter. Wakati haya yote yanatokea mke wa Paul Anita alikuwa akishuhudia.

Chanzo kiliongeza kuwa Peter anataka awe mhusika mkuu wa maswala ya fedha za kundi au apate mgao mkubwa zaidi, huku upande wa pili inadaiwa Paul anataka kaka yao mkubwa ambaye pia ni meneja wao Jude aendelee kuwa msimamizi mkuu wa maswala ya fedha zao kama ilivyokuwa miaka yote iliyopita, lakini mpaka ilifikia hatua ya kutaka wagawane mali kila mtu awe na chake.

Baada ya habari za ugomvi baina ya wana ndugu hawa kuenea, hii ni post ya Paul aliyoiandika juzi kupitia ukurasa wake wa Facebook.

“After the storm comes the calm. Hoping for better days ahead as one family. God’s intervention.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents