Bongo Movie

Sababu za Aunt Ezekiel kuanza na harusi kabla ya kitchen party na send-off!!

Wiki iliyopita picha za muigizaji wa filamu nchini, Aunt Ezekiel akifunga ndoa zilisambaa kwa kasi kwenye mtandao na kuzua maswali mengi kama iwapo amefunga ndoa kweli ama ni usanii tu. Wengi waliamini kuwa amefunga ndoa na wengi pia walikuwa na mashaka. Waliokuwa na mashaka walihisi si kweli kutokana na sababu zifuatazo.

1. Aunt Ezekiel alikuwa akiendelea kukusanya michango ya harusi iweje aamue kufunga ndoa wakati bado anachangisha?

2. Kwanini harusi yake isihudhuriwe na watu wake wa karibu hata kama ni ya kiislamu? (kutokana na picha hizo)

3. Aliwahi kuhojiwa na kudai kuwa angefunga ndoa mwezi November

Lakini ukweli uko wazi kuwa kumbe kweli picha hizo zilimaanisha kuwa tayari amefunga ndoa. Lakini kuna sababu za harusi yake kuwa hivyo.

“Ni mchumba wangu na hakika yeye ndiye mwenye maamuzi nikaamua nifanye hivyo,” ameiambia ‘Movie Leo’ ya Clouds FM. “Naweza sema bado yaani siko sawa mpaka nihakikishe hivyo vitu vyote vimeenda vimepita salama manake unajua shughuli yoyote hata kama ndogo lakini lazima unajua yaani unakaa ni pressure yaani sijui itakuaje sijui itakuwa vipi? Kwahiyo naweza kusema kwasababu ni mwanzo kwahiyo bado kiukweli naona yaani huko mbele kutakuaje.”

Kutokana na kufanya mchakato wake ‘kiflashback’ yaani kuanza na hatua ya mwisho ya harusi na kurudi nyuma, muigizaji huyo pia ameelezea jinsi Kitchen Party za Send-off zitakavyokuwa, “nataka nifanye vitu vya tofauti na kila kitu nataka kiwe tofauti na vile watu ambavyo wamezoea kuviona au wamewahi kwenda , kwahiyo mwisho wa siku nikisema niseme itakuaje, itakuwa hivi itakuwa hivi naweza nikawa nimezusha ugomvi.”

And by the way sasa jina lake ni Rahma baada ya kubadilisha dini na kuwa muislamu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents