Burudani

Sababu 10 za kwanini muziki wa Vanessa Mdee utavuka ‘boda’ mapema!!!

By  | 

vEE COVER

So imeshaeleweka kuwa ile single ya kwanza ya Vanessa Mdee iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu ‘Closer’ inatarajiwa kuzinduliwa Ijumaa hii katika party mahsusi (exclusive) iliyoandaliwa kwaajili ya kuisikiliza kwa mara ya kwanza.

Katika party hiyo ya kiVIP maceleb kibao wa Tanzania wamealikwa na bila shaka itakuwa miongoni mwa ‘listening party’ za kihistoria katika muziki wa Tanzania. Katika makala yetu ya mwishoni mwa mwaka jana ya ‘Wasanii 10 wa Tanzania wa kuwaangalia mwaka 2013’ Vanessa alikuwa miongoni mwa wasanii tuliowaweka kwenye list. Wakati akijiandaa kuzindua rasmi single yake ya kwanza, hizi ni sababu 10 za kwanini tunaamini mtangazaji huyu aliyeingia kwenye muziki hatachelewa kuuvukisha muziki wake kimataifa.

1. Ametoka katika muda muafaka

Ujio wa Vanessa Mdee kimuziki umekuwa wa kushtukiza hasa kwa watu wengi ambao walikuwa hawajui kama ana uwezo wa kuimba. Kwa muda mrefu msanii wa kike aliyekuwa akifanya vizuri kwenye muziki wa aina ya Vee ni Sara Kaisi aka Shaa. Kwa aina ya muziki anaofanya Shaa kulikuwa na wasichana wachache wa kumlinganisha naye ama hakuna kabisa. Ujio wa Vanessa umekuwa katika muda muafaka ambao muziki wa Tanzania ulikuwa unahitaji msanii mwingine wa kike mwenye taste na muonekano wa kimataifa.

Vee na Rick Ross

Vee na Rick Ross

2. Hajakurupuka

Katika nyimbo mbili ambazo Vee ameshirikishwa ni rahisi kung’amua uwezo na kipaji alichonacho msichana huyu. Si msanii anayetaka kuimba kwaajili ya kupata umaarufu bali anaimba kwakuwa anaweza na damu ya muziki iliyochemka mwilini mwake inamsukuma kufanya hivyo. Huwezi kumfananisha Vanessa na baadhi ya waigizaji wa kike wa filamu nchini walioingia kwenye muziki hivi karibuni. Wengi hufanya hivyo kwaajili ya kupata shows na kujipatia fedha. Ni rahisi kuwafahamu wasanii wa aina hiyo lakini si Vanessa.

3. Ana support ya watu wenye connection za kimataifa

Vee akiwa na Akon

Vee akiwa na Akon

Tangu asikike kwenye single mbili, Money ya AY na Me and You ya Ommy Dimpoz, Vee amekuwa akipokea mashavu kibao kutoka kwa watu wenye connection za kimataifa. Watu kama AY na Hermy B ambao wamekuwa naye bega kwa bega wanaweza kumsaidia kumfikisha mbali.

vee na omy

4. Ana mvuto wa asili (charisma)

Ukianzia kwa kazi yake kama mtangazaji, Vee amekuwa na fanbase kubwa mno ndani na nje ya Tanzania. Uwezo wake katika fani hiyo umemrahisishia kueleweka haraka katika career yake ya muziki aliyoianza hivi karibuni.

5. Ana muonekano na level za kimataifa

Vanessa-Mdee1

Ukimsikiliza Vee akiongea kwenye radio kwa mara ya kwanza unaweza kuhisi ni mmarekani ama si mtanzania. Kufanya kazi kwenye televisheni ya kimataifa ya MTV Base imemweka kwenye kundi la maceleb wa kimataifa.

6. Uwezo mzuri katika Ngeli

Sababu hii inatilia mkazo sababu ya tano. Tunafahamu Kiingereza ni tatizo kubwa kwa wasanii wengi wa Tanzania na ni sababu moja wapo inayokwamisha maendeleo ya muziki wetu nchi za nje kwakuwa wasanii hushindwa kupanua wigo wao kimataifa kwa kushindwa kujieleza vizuri kwa kimombo. Hicho si kikwazo kwa Vee.

7. Faida ya kufanya kazi MTV Base

Akiwa na rais wa zamani wa Nigeria, Obasanjo

Akiwa na rais wa zamani wa Nigeria, Obasanjo

Kupitia miradi kadhaa ya MTV Base kama MTV Base MEETS with MTN ambapo vijana hukutanishwa na watu maarufu duniani, Vanessa ambaye amewahi kuongozana na baadhi ya vijana wa Afrika amefanikiwa kukutana na wasanii wakubwa na wadau wa muziki wakiwemo Russell Simmons na Akon. Kwa kufanya kazi na kituo hicho, Vee ana uhakika wa kukutana na wasanii wengine wengi wakubwa duniani ambao ni rahisi kumpa mashavu.

8. Hatabiriki na amejipanga

Ukiangalia jinsi anavyofanya muziki wake, utagundua kuwa Vee amejipanga. Kuanzia namna alivyosubiri mpaka kuachia wimbo wake mpya na namna anavyopanga mambo yake, ni wazi kuna timu kubwa nyuma inayokuna vichwa kuhakikisha anatusua. Si wasanii wote hata wakubwa wenye desturi ya kufanya listening party. Ni kitu kinachotumia gharama kubwa na ili kufanikisha lazima ujipange kwanza.

9. Ni mrembo

Vee muonekano

Ni rahisi mno kwa msanii wake kike mwenye nzuri kufanikiwa kama akiwa mrembo and Vanessa has that look. Ni mrembo na anavutia kwenye video.

10. Anaweza kurap na kuimba

Si haki kumfananisha na Nicki Minaj kwakuwa hawaendani hata kidogo lakini ni sawa kumfananisha Vee na Lauryn Hill kwakuwa wote wana uwezo wa kurap na kuimba pia.

Muda ndio utakaoongea. Tunaisubiri kwa hamu Closer!1

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments